Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:16

Takwimu zaonyesha manunuzi ya siku ya Black Friday yashika kasi Afrika


Wateja wakiwa katika Duka la Macy la nguo, viatu na mabegi wakati wa usiku wa Black Friday, Nov. 29, 2019, in New York.
Wateja wakiwa katika Duka la Macy la nguo, viatu na mabegi wakati wa usiku wa Black Friday, Nov. 29, 2019, in New York.

Map of countries in Africa where U.S. Assistant Secretary of Commerce for Industry & Analysis Marcus Jadotte will travel in March 2016.
Map of countries in Africa where U.S. Assistant Secretary of Commerce for Industry & Analysis Marcus Jadotte will travel in March 2016.


Usifikirie juu ya sikukuu ya Thanksgiving ambayo Wamarekani wanaonyesha shukrani zao kwa vitendo kwa kukaribishana chakula na familia kukutana na kufurahia uwepo wao.

Barani Afrika, walaji au wateja hawashughulishwi na chakula cha usiku kikiwa na bata mzinga na vioja vingine vya familia.

Badala yake wako katika mkusanyiko mkubwa, wanasheherekea hafla zinazokuja baada ya siku hiyo ikiwemo siku ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ya Black Friday na baadaye sikukuu ya Christmas.

Makadirio ya Tovuti zenye kutangaza biashara siku ya Black Friday (Ijumaa) zinakadiria kwamba mauzo ya siku hii yako asilimia 1,331 juu zaidi kwa wastani wa mauzo ya siku nchini Nigeria na asilimia 1,952 juu zaidi nchini Afrika Kusini, uchumi mkubwa zaidi wa nchi hizo mbili katika bara la Afrika.

Nchini Nigeria, mteja wa wastani katika siku ya Black Friday anatumia kiasi cha dola za Marekani 60 ; nchini Afrika Kusini, ni mara mbili ya kiwango hicho kwa matumizi ya mteja.

Africa Kusini mchumi Mike Schussler, ambaye anakadiria kuwa siku hii ya Black Friday inayofuatiliwa imekuwa ikisheherekewa Africa Kusini kwa takriban muongo mmoja.

Anasema anafikiria Black Friday “imekuwa sasa kwa namna fulani ni yenye kuvuma dunia nzima. Hasahasa, nafikiri katika nchi wateja wanahitajika sana na wafanyabiashara wa rejareja, ambao wamelazimika kuwavutia wateja kutokana na kuwa wagumu kutumia madukani. Na Afrika Kusini na sehemu nyingine chache, mwisho wa mwezi Novemba kwa kawaida ni kipindi ambacho watu wanapata kile kinachoitwa malupulupu ya mwisho wa mwaka.”

XS
SM
MD
LG