Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:55

Mandela yuko hali mahtuti


Polisi wasimama nje ya Mediclinic Heart Hospital ambapo rais wa zamani Nelson Mandela anatibiwa mjini Pretoria,Juni 23, 2013.

Hali ya rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela yaripotiwa kudhoofika zaidi.

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela aripotiwa kuwa katika hali mahtuti. Msemaji wa rais Jacob Zuma Mac Maharaj aliiambia Sauti ya Amerika Jumapili jioni kuwa madaktari walimweleza rais Zuma kwamba hali ya bwana Mandela ni mbaya, wakati alipokwenda kumtembelea rais huyo wa zamani hospitalini.

Madaktari hao walisema afya ya mzee Mandela iliendeleea kudhoofika katika muda wa saa 24 zilizopita. Maharaj alisemaji rais Zuma alikuwa amefuatana hospitalini na bwana Cyril Ramaphosa naibu wa chama tawala cha African National Congress na baadaye rais huyo akatoa taarifa kuelezea umma kuwa madaktari wanafanya kila juhudi kuimarisha hali ya afya ya Madiba.

Wiki mbili zilizopita gari lililombeba bw. Mandela liliharibikia njiani na kulazimisha rais huyo mstaafu kuhamishiwa katika gari lingine kuelekea hospitali.

Chama kikuu cha upinzani Democratic Alliance, Jumapili kiliomba upelelezi kamili ufanywe juu ya kuharibika kwa gari hilo. Lakini bw. Maharaj anasema hakuna wakati wowote ambapo afya ya bw. Mandela ilipuuziliwa au kuhatarishwa.

Rais Zuma amewasihi raia wa Afrika Kusini na dunia kwa jumla waendelee kumwombea mzee Mandela na familia yake.
XS
SM
MD
LG