Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 22:58

Kitukuu wa Mandela azikwa


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ahudhuria maziko ya kitukuu wake Alhamisi huko Johannesburg.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, watoto wa shule na maafisa wa serikali ya Afrika Kusini walihudhuria Alhamisi maziko ya kitukuu wa Mandela, Zenani Mandela, aliyekufa katika ajali ya gari wiki iliyopita.

Wanafunzi wenzake Zenani, aliyekuwa na umri wa miaka 13, waliimba nyimbo za kwaya katika kanisa mjini Johannesburg.

Mandela mwenye umri wa miaka 91, ambaye hutokea hadharani mara chache, alikaa katika safu ya mbele kabisa kanisani hapo. Mke wake Graca Machel na mke wake wa zamani Winnie Madikizela-Mandela pia walihudhuria maziko hayo.

Zenani Mandela aliuawa katika ajali ya gari akiwa anarudi nyumbani kutoka katika tamasha la muziki la ufunguzi wa Kombe la Dunia mjini Johannesburg Ijumaa iliyopita.

XS
SM
MD
LG