Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:13

Mandela alazwa hospitali Johannesburg


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na mkewe Graca Machel nyumbani kwake Johannesburg, May 16, 2011.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na mkewe Graca Machel nyumbani kwake Johannesburg, May 16, 2011.

Mandela alazwa hospitali baada ya kupelekwa kupinwa tatizo la muda mrefu la tumbo.

Msemaji wa chama tawala cha Afrika Kusini Keith Khosa anasema, mtetezi mkuu wa kupinga ubaguzi mwenye umri wa miaka 93, amelazwa hospitali kutokana na mpango wa awali wa kwenda kupimwa na hakuna mpango wowote wa kupasuliwa.

Anasema hakuna haja ya kuwa na wasi wasi, kwani kiongozi huyo wa zamani ni mchangamfu. Hii ni mara ya pili kupelekwa hospitali katika muda wa mwaka mmoja.

Rais Jacob Zuma ailiwasilisha salamu za wananchi wa Afrika Kusini kumtakia afya njema na pia kuwataka watu kuheshimu faragha ya Bw Mandela na familia yake.

Madiba jina mashuhuri la kiongozi huyo wa zamani, mshindi wa tunzo ya Amani ya Nobel mwaka 1993, hajaonekana hadharani tangu mashindano ya Kombe la Dunia la kandanda nchini Afrika Kusini kutokanana na hali yake ya afya.

XS
SM
MD
LG