Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:14

Mamilion wahudhuria Misa ya Papa Francis Manila

Papa Francis kiongozi wa Kanisa la Roman Katoliki
Papa Francis kiongozi wa Kanisa la Roman Katoliki

Ufilipino ina waumini wa Kanisa la Roman Katoliki wapatao milioni 80 na ndiyo nchi yenye Wakatoliki wengi barani Asia.

Kiongozi wa Kanisa la Roman Katoliki Papa Francis, aliongoza Misa kwa mamilioni ya raia wa Ufilipino waliokusanyika katika uwanja wa Rizal mjini Manila licha ya mvua leo Jumapili, hii ikiwa siku yake ya mwisho ya ziara yake huko Ufilipino.

Mamlaka nchini humo zinasema zaidi ya watu milioni sita walihudhuria Misa hiyo, idadi hiyo ikipita kwa milioni moja mkusanyiko wa waumini waliohudhuria Misa iliyoongozwa na marehemu Papa John Paul wa Pili katika uwanja huo, huo wa Rizal mwaka wa 1995.

Ufilipino ina waumini wa Kanisa la Roman Katoliki wapatao milioni 80 na ndiyo nchi yenye Wakatoliki wengi barani Asia.

XS
SM
MD
LG