Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 18:33

Mamilioni wapiga kura katika uchaguzi wa rais Misri.


Wamisri wakisimama kwa mistari mirefu kushiriki katika uchaguzi wa rais wa kihistoria mjini Cairo, May 23 2012.

Mamilioni wajitokeza katika uchaguzi wa kwanza wa rais tangu rais Honi Mubarak aondolewe madarakani kwa mapinduzi.

Mamilioni ya Wamisri walijipanga kwenye mistari mirefu jumatano kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa rais tangu rais Hosni Mubarak kujiuzulu mwaka jana kati kati ya upinzani mkubwa.

Maandalizi ya uchaguzi huo wenye mvutano mkali kwa kiasi kikubwa unawahusisha wagombea unawahusisha wale ambao wana uhusiano na bwana Mubarak dhidi ya Waislam wanaojaribu kuunda ushirikiano mpya. Kwa jumla wagombea 13 wako kwenye karatasi ya kura lakini mmoja amejitoa kwenye kinyang’anyiro . Uchaguzi utakuwa wa siku mbili.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Elizabeth Arrot alikuta makundi makubwa ya watu kwenye vituo vya kupigia kura vya Cairo.

Kiasi cha Wamisri milioni 50 wanastahili kupiga kura . Miongoni mwao ni Gihad Amr ambaye anasema hajui atarajie nini.

Huku maandamano makubwa yakiendelea wiki kadhaa kabla ya uchaguzi kumekuwa na wasi wasi kuhusu ghasia.

Mashirika ya habari yanasema Polisi mmoja alipigwa risasi na kuuwawa nje ya kituo cha kupigia kura mjini Cairo kwenye mapigano kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa nafasi ya urais.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG