Mamia ya watunisia wameandamana katika mji mkuu Tunis kupinga ghasia na vurugu kufuatia wimbi la maandamano katika siku chache zilizopita, ambapo moja ya maandamanao hayo yalipelekea kuuwawa kwa bahati mbaya kwa risasi kwa mtoto wa miaka 14.
Karibu darzeni ya vyama vya siasa waliandaa maandamano ya alhamisi na kutaka kipindi cha mpito cha kidemokrasia cha amani.
Maandamano hayo hayakuhusisha chama cha Kiislam cha Ennahdha kinachofikiriwa kuwa na msimamo wa wastani lakini kimelaumiwa na baadhi kwa kuchochea vurugu. Kundi hilo limekana kuhusika kwa njia yeyote katika ghasia za hivi karibuni.