Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:12

Mama Teresa atangazwa kuwa mtakatifu


Mama Teresa wakati wa uhai alitumikia masikini.
Mama Teresa wakati wa uhai alitumikia masikini.

Papa Francis alimtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu katika mwaka aliotangaza mtakatifu wa huruma siku ya Jumapili wakati wa hafla ya kumtangaza mbele ya maelfu ya watu.

“Kwa heshima ya Utatu mtakatifu tunamtangaza mbarikiwa Teresa wa Calcutta kuwa mtakatifu na kumuoredhesha kati ya watakatifu tukitangaza na kanisa lote kwa heshima kubwa” alisema kiongozi huyo wa kanisa katoliki kwa lugha ya Kilatini.

Mama Teresa mshindi wa nishani ya nobel alijulikana wakati wa uhai wake kama mtakatifu wa masikini kwa kazi yake miongoni mwa walio na umasikini mkubwa nchini India na kuwasili Calcutta January 6,1929.

XS
SM
MD
LG