Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:57

Malkia Elizabeth agundulika ana Covid 19


Makopo ya chai yakiwa na picha ya Malkia Elizabeth madukani baada ya kutangazwa kuwa amekutwa na Covid 19.
Makopo ya chai yakiwa na picha ya Malkia Elizabeth madukani baada ya kutangazwa kuwa amekutwa na Covid 19.

Malkia Elizabeth, mwenye umri wa miaka  95, amepimwa na kukutwa na  COVID-19 lakini ana dalili ndogo za ugonjwa huo na anatarajia kuendelea na majukumu mepesi wiki hii, Buckingham Palace ilisema Jumapili.

"Malkia leo amepimwa na amekutwa na COVID," ofisi ya Malkia ilisema. "Malkia ana dalili ndogo za ugonjwa huo lakini anatarajia kuendelea na kazi nyepesi huko Windsor katika wiki ijayo."

"Ataendelea kupata matibabu na atafuata miongozo yote inayofaa," ofisi hiyo ilisema.

Charles, mwenye umri wa miaka 73, mrithi wa kiti cha enzi, mapema mwezi huu alijiondoa kwenye hafla moja baada ya kuambukizwa corona kwa mara ya pili. Chanzo cha ofisi ya kifalme kilisema kuwa alikutana na malkia siku chache zilizopita.

Afya ya malkia huyo,mkongwe na aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani, imekuwa ikiangaliwa tangu alipolazwa hospitali Oktoba mwaka jana kwa maradhi ambayo hayakutajwa na kisha kushauriwa na madaktari wake kupumzika.

XS
SM
MD
LG