Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:38

Mali yawakamata wanajeshi 49 wa Ivory Coast, ikidai ni mamluki


Kanali Assimi Goita, kiongozi wa kijeshi wa Mali, Agosti 22, 2020. Picha ya AP
Kanali Assimi Goita, kiongozi wa kijeshi wa Mali, Agosti 22, 2020. Picha ya AP

Mali imesema wanajeshi 49 kutoka Ivory Coast walikuwa mamluki baada ya kuwamakata wanajeshi hao walipowasili nchini humo, serikali ya Mali imesema Jumatatu.

“Imethibitishwa kuwa wanajeshi 49 wa Ivory Coast walikuwa kwenye ardhi ya taifa ya Mali kinyume cha sheria,” msemaji wa serikali Abdoulaye Maiga amesema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya serikali, akiwaita watu hao “mamluki”.

“Serikali ya mpito imeamua kuwasilisha kesi hiyo kwenye mamlaka husika ya mahakama.”

Awali, mwanadiplomasia wa Ivory Coast alisema baadhi ya wanajeshi hao walipelekwa kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa mataifa wa kulinda usalama (MINUSMA). Kikosi hicho kimesema kinaamini wanajeshi hao walikuwa katika kitengo ambacho kinatoa msaada wa kimkakati kwa kikosi cha jeshi la Ivory Coast chini ya ujumbe wa MINUSMA.

XS
SM
MD
LG