Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:12

Mali yasitisha kubadilishana zamu wanajeshi wa kulinda amani wa UN


Wanajeshi wa Ivory Coast wa tume ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani nchini Mali( MINUSMA), August 7, 2019. Picha ya AFP
Wanajeshi wa Ivory Coast wa tume ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani nchini Mali( MINUSMA), August 7, 2019. Picha ya AFP

Mali Alhamisi imesema kwamba inasitisha kubadilishana zamu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kwa sababu za 'usalama wa kitaifa,' katika mvutano mpya kati ya utawala wa kijeshi wa Mali na washirika wake wa kimataifa.

Zowezi la kubadilishana zamu la kikosi cha MINUSMA limesitishwa, ikiwa ni pamoja na duru iliyokwisha pangwa kufanyika, wizara ya mambo ya nje mjini Bamako imesema.

Katika taarifa yake wizara hiyo imesema kwamba kusitishwa huko kutaendelea hadi utapofanyika mkutano wa kurahisisha uratibu na ukaguzi wa kubadilishana zamu wanajeshi.

Taarifa hiyo haikufafanua sababu za hatua hiyo.

Lakini inatokea siku nne baada ya Mali kuwakamata wanajeshi 49 wa Ivory Coast iliowaelezea baadaye kuwa ni mamluki ambao walikuwa na lengo la kuipindua serikali inayoongozwa na jeshi.

Ivory Coast ilisema wanajeshi hao ni kutoka kitengo kinachochangia kwa kulinda usalama wa taifa ( NSE), utaratibu wa Umoja wa mataifa unaoruhusu vikosi vya kulinda amani kutumia wakandarasi wa nje kwa shughuli za kijeshi.

Wanajeshi hao ambao walikamatwa baada ya kuwasili mjini Bamako wakiwa ndani ya ndege maalum, walikuwa katika mzunguko wa nane chini ya utaratibu huo, kwa mujibu wa Ivory Coast.

XS
SM
MD
LG