Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 22:28

Mali yaanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yanayodaiwa kufanywa na mamluki wa Russia


Picha ya video iliyopatikana kutoka jeshi la Ufaransa April 22, 2022, ambalo linadai kuirekodi kwa kutumia ndege isiyo na rubani, inaonyesha kulingana na jeshi hilo, mamluki wa Russia wakizika miili karibu na kambi ya Gossi, kaskazini mwa Mali. Picha ya AFP
Picha ya video iliyopatikana kutoka jeshi la Ufaransa April 22, 2022, ambalo linadai kuirekodi kwa kutumia ndege isiyo na rubani, inaonyesha kulingana na jeshi hilo, mamluki wa Russia wakizika miili karibu na kambi ya Gossi, kaskazini mwa Mali. Picha ya AFP

Jeshi la Mali Jumanne limetangaza kwamba uchunguzi umeanzishwa kuhusu kaburi la pamoja lililogunduliwa karibu na kambi ya zamani ya jeshi la Ufaransa, ambapo Paris imesema wanajeshi wa Russia walizika maiti hizo.

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kijeshi ambaye ameanzisha uchunguzi huo kwa agizo la wizara ya ulinzi, alitembelea kituo cha Gossi mashariki mwa nchi hapo tarehe 23 Aprili.

Taarifa rasmi imesema “atatafuta ukweli wa ushahidi wote” wa kesi hiyo na atawafahamisha wanainchi kikamilifu.

Tarehe 21 Aprili, siku mbili baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuikabidhi tena kambi hiyo kwa Mali, walitoa video inayosemekana inawaonyesha mamluki wa Russia wakizika maiti karibu na kambi hiyo ili kuwashtumu kwa uwongo wanajeshi wa Ufaransa wanaoondoka.

Katika video hiyo iliyorekodiwa na ndege isiyo na rubani, wanajeshi wa Russia wanaonekana wakifunika maiti na mchanga karibu na kambi ya Gossi.

Ufaransa ilikabidhi rasmi udhibiti wa kambi ya Gossi kwa Mali Jumanne iliyopita kama sehemu ya mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa uliotangazwa mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG