Taarifa ya msemaji wa serikali ya Mali Abdoulaye Maiga, imesema kwamba hatua ya kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita, ya kuwaachilia huru wanajeshi hao wa Mali ni uthibitisho kwamba anachukua hatua za kuleta amani na kuweka mazingira ya kufanyika mazungumzo, na kuimarisha uhusiano kati ya Mali na nchi nyingine hasa Mali na Ivory Coast.
Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya wanajeshi 46 kati ya 49, kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.
Wanajeshi wengine watatu, ambao wote ni wanawake, waliachiliwa mnamo mwezi Septemba. Kesi dhidi yao ilisikilizwa bila yao kuwepo mahakamani na kuhukumiwa kifo.
Wanajeshi 49 wa Ivory Coast walikamatwa mwezi Julai walipokuwa wanafanyia kazi shirika la huduma za safari za anga la Sahel, shirika la binafsi ambalo linafanya kazi nchini Mali, kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.
Serikali ya Mali ilikuwa imepewa hadi Januari Mosi kuwaachilia huru wanajeshi hao. Amri hiyo ilitolewa na viongozi wa Afrika Magharibi.