Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:15

Mali imesema haitaheshimu vikwazo vya ECOWAS


Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa Mali kanali Assimi Goita wakati wa kikao na viongozi wa ECOWAS April 5 2022. Picha : AP

Serikali ya Mali imesema kwamba haitatekeleza vikwazo vya jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS, dhidi ya Guinea.

Vikwazo hivyo viliwekwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka uliopita, na kutokana na utawala wa kijeshi wa Guinea kuchelewa kuandaa uchaguzi mkuu.

Maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Guinea waliwekewa vikwazo Pamoja na mali yao. Wamepigwa marufuku ya kusafiri katika nchi wanachama wa Ecowas.

Msemaji wa waziri mkuu wa Mali Abdoulaye Maiga amesema kwamba kwa kuzingatia ushirikiano mwema kati ya Mali na Guinea, serikali ya mpito ya Mali haitatekeleza vikwazo dhidi ya Guinea.

Amesema kwamba Mali itachukua hatua za kuisaidia Guinea kukabiliana na vikwazo hivyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG