Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 00:33

Washtakiwa wa kashfa ya Cashgate Malawi wafikishwa mahakamani


Waziri wa zamani wa sheria nchini Malawi, Ralph Kasambara

Mahamaka moja nchini Malawi imemkuta na hatia waziri wa zamani wa sheria na watu wengine wawili kwa njama za kutaka kumuuwa mkurugenzi wa zamani wa bajeti katika wizara ya fedha hapo mwaka 2013. Tukio hilo lilifichua kashfa ya rushwa iliyojulikana kama Cashgate, ambayo ilipelekea takriban wafanyabiashara 70 na maafisa wa serikali kukamatwa.

Paul Mphwiyo alinusurika kupigwa risasi kwenye shavu hapo September mwaka 2013 alipokuwa akiendesha akienda nyumbani kwake mjini Lilongwe.

Siku chache baadae polisi walimkamata waziri wa zamani wa sheria,Raphael Kasambara, mwanajeshi wa zamani wa Malawi Macdonald Kumwembe na mfanyabiashara Pika Manondo kwa kushiriki katika shambulizi hilo.

Kasambara alishutumuiwa kupanga njama za kumuuwa Mphiwiyo huku Kumwembe na Manondo walikabiliwa na mashtaka mawili ya kujaribu kuuwa kadhalika kwa kupanga njama za kuuwa.

Walikana mashtaka hayo wakati wa kesi yao ambayo waendesha mashtka waliwasilisha zaidi ya mashahidi 15.

Hakimu wa mahakama kuu Michaeal Mtambo, alitowa hukumu alhamisi kwa kusema baada ya kuchambua ushahidi katika kesi hiyo amewakuta na hatia. Na dhamana kwa watuhumiwa wote watatu inaondolewa na wataendelea kubaki rumande.

Alipokuwa anachukuliwa ndani ya gari la polisi kwenda jela, Kasambara alisema hukumu ilihujumiwa na washtakiwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Mphwiyo aliyenusuruka kupigwa risasi, anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika kashfa ya dola millioni 32 katika kadhia ya Cashgate. Alikamatwa mwaka 2014 kwa shutuma ya kufanya biashara haramu ya mzunguko wa fedha , wizi na njama ya kukwepa sheria. Mke wake pia ameshtakiwa kwa biashara haramu ya mzunguko wa fedha na wizi.

Bado tarehe haijawekwa ya kutolewa hukumu ya kifungo.

XS
SM
MD
LG