Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:55

Malawi yashangazwa Marekani kuondoa msaada wa kifedha


Polisi wa Malawi wakifanya doria katika mji wa lilongwe
Polisi wa Malawi wakifanya doria katika mji wa lilongwe

Kufuatia ghasia zilizozuka wiki iliyopita Marekani imeondoa msaada wa dola milioni 350 nchini Malawi

Serikali ya Malawi imesema imeshangazwa na Marekani kuondoa msaada wake wa dola milioni 350 kufuatia ghasia zilizokuwa na mauaji baina ya polisi na waandamanaji wiki iliyopita.

Ushirikiano wa maendeleo ya millennia –MCC, shirika la Marekani ambalo linasaidia nchi zinazoendelea limesema litatathmini kama lisimamishe au kuondoa kabisa msaada huko Malawi baada ya watu 18 kufariki dunia wakati wa ghasia zilizizozuka katika miji mitatu nchini humo.

Msemaji wa rais Bingu Wa Mutharika amesema shirika hilo la MCC ilitangaza uamuzi wake wa kuondoa msaada wa kifedha Jumanne kabla ya kusikia maelezo ya mambo yaliyotokea kwenye eneo la matukio.

Heatherwick Ntaba ameimbia VOA kuwa watu waliouwawa Jumatano iliyopita na Alhamisi walikuwa wahalifu ambao hawakuwa sehemu ya maandamano ya amani.

Waandamanaji walikuwa wanapinga upungufu wa mafuta, ongezeko la bei na ugumu wa maisha nchini humo.

XS
SM
MD
LG