Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 12:40

Malawi yafunga mipaka yake kwa siku 14 kutokana na Corona


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera

Malawi imetangaza kufunga mipaka yake kwa siku 14 ili kuzuia mikusanyiko ya watu baada ya kuripotiwa ongezeko jipya la maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Baada ya karibu miezi miwili ya kutoripoti kisa chochote cha maambukizi ya virusi vya Corona, Malawi imesema kwamba imerekodi visa 46, na kufikisha idadi ya watu 6,248 ambao wameambukizwa virusi hivyi nchini humo.

Kulingana na wizara ya afya ya Malawi, watu 187 wamefariki dunia.

Mipaka ya Malawi na viwanja vya ndege vilifunguliwa Oktoba baada ya kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona kupungua, japo baadhi ya wataalam wanasema kwamba huenda idadi kamili ya maambukizi ikawa kubwa sana kwa sababu watu 80,000 pekee ndio wamefanyiwa vipimo.

Malawi ina jumla ya watu milioni 19.

Kamati maalum iliyoundwa na rais kushughulikiwa maambukizi ya virusi vya corona, imesema mjini Lilongwe kwamba wafanyakazi muhimu pekee na magari ya kubeba bidhaa muhimu kama mafuta na dawa, ndiyo ataruhusiwa kuvuka mpaka.

Raia wa Malawi waliofurushwa kutoka nchi nyingine pia wataruhusiwa kuingia nchini humo lakini watalazimika kufanyiwa vipimo vya Corona.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG