Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 16:02

Malawi kushiriki Olimpiki ya 2020


Baadhi ya wasichana waliojitokeza kwenye uwanja wa Zomba nchini Malawi mwishoni mwa wiki.

Malawi imeelekeza macho yake kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020 wakati ikizindua zoezi la kuwatafuta wasichana wadogo wenye kipaji cha kucheza mpira wa miguu.

Malawi imeelekeza macho yake kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020. Nchi hiyo haijawahi kufuzu kushiriki kwenye michezo hiyo lakini wanariadha wake wamekuwa wakishiriki kwa misingi ya mshikamano na mataifa mengine.

Serikali pamoja na chama cha kandanda wananuia kubadilisha hilo. Mwishoni mwa wiki zoezi la kutafuta wachezaji wenye vipaji miongoni mwa wasichana wenye umri kati ya miaka 6 na 12 limeanza.

Kulikuwa na shangwe na nderemo wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Zomba uliofadhiliwa na shirika la soka duniani FIFA kupitia program iliopewa jina Girls Grassroot Festival ambapo takriban wasichana 300 walishiriki.Zaidi ya wachezaji 40 wachanga walichaguliwa.

XS
SM
MD
LG