Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:36

Malawi kutumia kliniki za kwenye gari kutoa chanjo za Covid


Mkazi wa Malawi apokea chanjo kwenye mji mkuu wa Blantyre.
Mkazi wa Malawi apokea chanjo kwenye mji mkuu wa Blantyre.

Mamlaka za afya nchini Malawi Jumatano zimesema kwamba kusita kwa watu kupokea chanjo za Covid nchini humo huenda kukapelekea maelfu ya dozi kuharibika ifikapo mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kufikia sasa ni asilimia 2 pekee ya watu nchini humo waliopokea chanjo hizo,wakati serikali ikisema kwamba inapanga kubuni kliniki za kwenye magari zitakazoweza kuwafikia watu wa vijijini.

Kufikia sasa, Malawi imepokea zaidi kidogo ya dozi milioni 1.2 za chanjo aina ya Johnson& Johnson pamoja na AstraZeneca, chini ya mpango unao ongozwa na shirika la afya duniani wa COVAX.

Hata hivyo watu wanasita kupatiwa chanjo hivo nchini humo kwa kiasi kikubwa kwasababu ya dhana potofu kuhusiana na ufanisi na usalama wake.Dkt Gift Kawalazira, anayeongoza idara ya huduma za afya na kijamii kwenye ofisi ya afya mjini Blantyre anasema kwamba kuna sababu nyingine kwa kiwango kidogo cha watu kupatiwa chanjo.

Anasema kwamba wamegundua kwamba, kadri msimu wa joto unavyokaribia, idadi ya maambukizi inapungua kwa kiwango kikubwa na kwa hivyo kusababisha idadi ya watu wanokuja kupokea chanjo kila siku kupungua kutoka watu 2,000, hadi takriban 400 kwa sasa.

Dkt Kawalazira anasema kwamba kuwepo kwa kliniki za kwenye magari kutasaidia kufikia watu wengi zaidi ,akiongeza kwamba baada ya mpango huo kuzinduliwa Jumamosi, watu zaidi ya 600 walipokea chanjo zao, wakati makampuni 6 binafsi yakiagiza kliniki hizo ili kutoa chanjo kwa wafanyakazi wao.

Mtaalam huyo wa afya anatabiri kwamba mpango huo utaiwezesha Malawi kufikia lengo lake la kutoa chanjo kwa asilimia 60 ya watu wake ifikapo mwaka ujao, ili pia kuondoa uwezekano wa chanjo kuharibika.

Mwezi Mei, Malawi iliteketeza takriban dozi 20,000 za AstraZeneca zilizokuwa zimeharibika baada ya watu wengi kukataa kuzipokea kwa wakati kutokana na wasiwasi wa usalama wake wakati huo.

Takwimu kutoka wizara ya afya ya Malawi zinasema kwamba kufikia sasa, takriban watu 700,000 wamepokea walau chanjo ya kwanza huku wengine 400,000 wakiwa wamepokea chanjo kamili, ikiwa ni asilimia 2.1 ya jumla ya watu milioni 18 nchini humo.

Ili kuharakisha zoezi hilo, Serikali inashirikiana na viongozi wa vijiji katika kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kupokea chanjo za covid mara baada ya kuona kliniki za kwenye magari zikija vijijini vyao.

XS
SM
MD
LG