Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:53

Malawi yachoma pembe za ndovu haramu


Pembe za ndovu haramu zikichomwa.
Pembe za ndovu haramu zikichomwa.

Shirika la wanyama pori la Afrika linasema kuwa ndovu takriban elfu 35 waliuwawa barani humo mwaka jana.

Malawi ilichoma pembe za ndovu takriban mia 8 jummatatu kuonyesha nguvu dhidi ya biashara haramu ya wanyama pori. Maafisa wa forodha walikamata pembe hizo mwaka 2013, pale zilipoingizwa kwa magendo nchini Malawi kutoka Tanzania.

Wafanyakazi wa mbuga ya wanyama walichoma moto takriban tani 2.6 za pembe za ndovu katika hifas=dhi ya mbuga ya Mzuzu kaskazini mwa Malawi.

Shehena ya pembe za ndovu ilikadiriwa kugharimu dola millioni 3.

Brighton Kumchedwa ni mkurugenzi wa mbuga za wanyama pori nchini Malawi.

Bw. Kunchedwa anasema kuwa, kile wanachojaribu kuonyesha ni kuwa ulanguzi wa pembe za ndovu hauna thamani kwa sababu kuna sharia ambayo inapiga marufuku biashara ya kimtaiafa ya pemb za ndovu. Kwa hiyo kile tunachosema ni kuwa, acha usafirishaji haramu wa bidhaa za wanyama pori hususan pembe za ndovu.

Pembe hizo za ndovu zilikamatwa mwaka 2013 lakini mahakama kuu ya Mzuzu iliwapatia maafisa ruhusa ya kuchoma pembe hizo mwezi huu. Tanzania awali ilizuia kuchomwa kwa pembe hizo, ikisema inahitaji baadhi ya pembe hizo kama ushahidi kwa wa kesi mahakamani nchini tanzania.

Ndugu wawili raia wa Malawi walikamatwa wakiwa na shehena ya pembe za ndovu. Walitozwa aini ya dola elfu 5 mia 5 kwa usafirishaji haramu wa pembe za ndovu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Malawi kuchoma pembe za ndovu walokamata. Hio inakuja kufwatia harakati banarani Afrika juu ya kuendelea kuuwawa kiharamu kwa ndovu.

Idara ya wanyama pori ya Malawi inaeleza kuwa Malawi imepoteza takriban nusu ya idadi ya ndovu walokuwa nao tangu mwaka 1980, hususan kutokana na uwindaji haramu. Taifa hilo limekuwa njiapanda kwa wasafririshaji haramu wa pembe.

Kumchedwa anasema serikali inashughulikia suala hilo sasa.

Kumchedwa anasema, pembe hizi zinatokea Tanzania kwa sababau sharia zetu ni dhaifu sana. Lakini hivi tunavyozungumza, tunatathmini sharia, ili ziwe na adhabu kali.

Biashara ya kimataifa ya pembe za ndovu ilisitishwa mwaka 1989, lakini wataalam wanasema uwindaji haramu wa ndovu umeongezeka ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya pembe za ndovu huko Asia.

Shirika la wanyama pori la Afrika, linasema kuwa ndovu takriban elfu 35 waliuwawa barani Afrika mwaka jana.

XS
SM
MD
LG