Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 00:22

Makundi ya waasi 53 yanashiriki mazungumzo ya amani DRC


Rais wa DRC Felix Tshisekedi (kushoto) akiwa na mjumbe wa amani kwa ajili ya DRC Uhuru Kenyatta
Rais wa DRC Felix Tshisekedi (kushoto) akiwa na mjumbe wa amani kwa ajili ya DRC Uhuru Kenyatta

Waakilishi wa makundi ya waasi 53 yanayopigana mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanahudhuria mazungumzo ya amani yanayoendelea Nairobi Kenya.

Mjumbe wa amani kwa ajili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa makundi hayo kutoa fursa ya juhudi za amani kufanikiwa na hali ya utulivu kurejea mashariki mwa DRC na kwamba makundi yote ya wapiganaji kutoka nje ya DRC yanastahili kuvunjwa mara moja na kurejea nchini mwao.

Waakilishi wa mashirika ya kijamii pia wanahudhuria mazungumzo hayo.

Waandalizi wa mkutano wa Nairobi wamesema kwamba makundi 53, likiwemo kundi la M23, yamekubali kusitisha vita.

Wanajeshi wa Burundi na Uganda wanapambana na makundi ya waasi yanayoshutumiwa kutoka nchini mwao na kujificha DRC.

DRC inadai kwamba waasi a M23 wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda, madai ambayo ripoti kadhaa zinaungana nayo, japo Rwanda imekanusha shutma hizo kila mara.

Kundi la M23 limekuwa likipigana sana na wanajeshi wa DRC, likidai kwamba linalinga maslahi ya watu kutoka jamii ya Tutsi dhidi ya dhuluma za serikali na mashambulizi ya makundi mengine ya waasi.

XS
SM
MD
LG