Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:34

Makundi ya haki za binadamu yanazungumzia siasa za Togo


Waandamanaji mjini Lome wanaoipinga serikali ya Togo. Sept. 6, 2017.
Waandamanaji mjini Lome wanaoipinga serikali ya Togo. Sept. 6, 2017.

Makundi ya kutetea haki za binadamu huko Togo yameonya kuhusu kuanza kwa kampeni ya kuwanyanyasa wanaharakati nchini humo kwa juhudi zao za kuwahamasisha wananchi kujiunga na malalamiko ya miezi kadhaa dhidi ya rais anaekabiliwa na misuko suko ya kisiasa Faure Gnassingbe.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Amnesty International, Front Line Defenders na Africa Rising inaeleza kwamba ni lazima maafisa wa usalama wa Togo waache kuwabughudhi wanaharakati wanaotetea demokrasia na walinda haki za binadamu kuhusiana na maandamano pamoja na malalamiko yanayoendelea kote nchini humo.

Wapinzani Togo wakishinikiza mageuzi ya katiba huko Lome, Sept. 7, 2017.
Wapinzani Togo wakishinikiza mageuzi ya katiba huko Lome, Sept. 7, 2017.

Taarifa inaeleza kwamba hali ya haki za binadamu imekua ikizorota nchini humo tangu kuzuka kwa maandamano ya kutetea demokrasia mwezi Agosti 2017. Upinzani nchini Togo unataka kuwepo na mihula miwili tu ya utawala wa rais na kuwepo na duru ya pili ya uchaguzi wa rais pindi inapotokea hakuna anaepata asilimia 51. Hatua hii ni katika kupinga mipango ya serikali kutaka kufanya mabadiliko ya katiba kumruhsu Rais Gnassingbe kugombania tena kiti cha rais.

Wananchi na wanaharakati wanamtaka kiongozi huyo kuachia madaraka kwani wamechoka kuona familia moja inaendelea kutawala taifa hilo la Afrika magharibi tangu lilipojinyakulia uhuru wake zaidi ya miaka 50 iliyopita.

XS
SM
MD
LG