Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 20, 2025 Local time: 07:37

Makundi hasimu ya Afghanistan, yadai kuuwa 50


Makundi mawili ya waasi wa Afghanistan, yanayoundwa na maafisa wa zamani wa serikali na maafisa wa kijeshi, yanadai kuwauwa maafisa na wanajeshi 50 wa Taliban, katika kipindi cha mwezi Novemba.

Wanambambo hao wa kushambulia kwa kushtukiza wamefanya mashambulizi makali kaskazini na kaskazini mashariki mwa nchi ambapo Taliban walipata upinzani mkubwa wakati wa utawala wao wa awali kuanzia 1996 hadi 2001.

Katika taarifa fupi ya lugha za Dari na Kiingereza iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, taasisi za Afghanistan Freedom Front na National Resistance Front zilidai kuwa wapiganaji wao huwakulenga wanachama wa Taliban, mara kwa mara kwenye vituo vya ukaguzi, kambi za kijeshi na hata kwenye barabara kuu.

Mpaka sasa, Taliban wamepunguza uasi kwa watu wenye silaha, wakisema amani na utulivu vimerejeshwa kikamilifu nchini kote.

Forum

XS
SM
MD
LG