Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 07:15

Makubaliano ya amani Ukraine yaingia dosari


Mwanajeshi wa Ukraine na vifaa vya kivita ndani ya mji wa Debaltseve, mashariki mwa nchi hiyo, Ferbuari 16, 2015.
Mwanajeshi wa Ukraine na vifaa vya kivita ndani ya mji wa Debaltseve, mashariki mwa nchi hiyo, Ferbuari 16, 2015.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa siku moja nchini Ukraine, yanaonekana kuvunjika leo Jumatatu.

Inaripotiwa kutokea mashambuliano baina ya wanaotaka kujitenga na kuungwa mkono na Russia, na majeshi ya Kyiv mjini Debaltseve.

Majibizano hayo yanadaiwa kutokea katika eneo la reli ambapo waasi wamezunguka vikosi vya Ukraine.

Waasi hao wamewapa wapiganaji wa Kyiv, sharti la kutoka nje katika mji huo kwa usalama, endapo tu wanajeshi wa Kyiv wataweka silaha zao chini.

Msemaji wa jeshi la Ukraine, Vladislav Seleznyov, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba walikataa shauri hilo.

Kwa mujibu wa Seleznyov, chini ya makubaliano ya kusimamisha mapigano, mji huo upo ndani ya mamlaka ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG