Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 14, 2022 Local time: 21:49

Makubaliano ya amani Sudan Kusini yatekelezwa


Wananchi wa Sudan Kusini wakishinikiza kuwepo amani katika nchi yao

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande mbili hasimu nchini Sudan Kusini yameanza kutekelezwa baada ya saa sita usiku Jumapili katika juhudi za hivi karibuni kumaliza vita iliyoleta maangamivu kwa kipindi cha miaka minne.

Serikali na vikundi venye silaha vilisaini makubaliano ya kusitisha mapigano Alhamisi wakati wa mazungumzo ya amani huko Addis Ababa, yaliyoanza kuanzia saa 00:01 (nyakati za Sudan Kusini) Disemba 24.

Makubaliano hayo yanaeleza kuwa pande zote husika za wapiganaji wanalazimika “kubakia katika vituo vyao maramoja” wasitishe harakati ambazo zinaweza kupelekea kupigana na kuwaachia wafungwa wa kisiasa pamoja na wanawake na watoto waliotekwa.

Riek Machar, makamu wa rais wa zamani ambaye kuhitalafiana kwake na Rais Salva Kiir , kulipelekea vita hiyo mnamo Disemba 2013, ameagiza vikosi vyake vya waasi “ kusimamisha mashambulizi yote”.

Katika tamko lililotolewa Ijumaa ameagiza vikundi vyote lazima “ vitulie katika vituo vyao na wanaweza tu kupigana kwa kujihami au watakapo kabiliwa na mashambulizi”.

Viongozi wa Sudan Kusini walipigana kwa miongo mingi kutafuta uhuru wao, lakini baada ya kupata uhuru huo mwaka 2011, kulikuwa na mvutano mkubwa wa kugombania madaraka baina ya Kiir na Machar na kupelekea vita kubwa ya wenyewe kwa wenyewe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG