Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:49

Makombora ya Russia yaua watu 22 katika mji wa Ukraine wa Vinnytsia


Moshi waonekana baada ya makombora ya Russia kuushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, June 5, 2022. Picha ya AP
Moshi waonekana baada ya makombora ya Russia kuushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, June 5, 2022. Picha ya AP

Idadi ya watu waliouawa katika mji wa Ukraine wa Vinnytsia ulioshambuliwa Alhamisi na makombora ya Russia, imefikia 22, huku wengine 100 wakijeruhiwa. Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine.

Polisi wamesema jengo la ofisi katikati mwa mji huo, lililoko umbali wa kilomita 270 kusini magharibi mwa mji mkuu, Kyiv, lilishambuliwa na makombora matatu.

Makombora hayo ambayo yalirushwa kutoka manwari ya Russia katika bahari nyeusi, yaliharibu majengo ya makazi katika eneo hilo na kuteketeza magari 50 yaliyokuwa yameegeshwa karibu na eneo hilo.

Gavana wa jimbo la Vinnytsia, Serhiy Borzov, amesema vifaa vya ulinzi wa anga ya Ukraine vilidungua makombora mengine manne juu ya eneo hilo.

Vinnytsia ni mmoja ya miji mikubwa ya Ukraine, ukiwa na wakazi 370,000. Maelfu ya watu kutoka mashariki mwa Ukraine, ambako Russia imejikita zaidi katika mashambulizi yake, walikimbilia kwenye mji huo wa Vinnytsia tangu kuanza kwa vita tarehe 24 Februari.

Umoja wa mataifa umesema watoto watatu ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio la Vinnytsia.

XS
SM
MD
LG