Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:24

Korea Kaskazini yaendelea kukaidi vikwazo


Korea Kaskazini haikutangaza eneo la marufuku ya usafiri wa meli kabla ya kufyetua makombora hayo ingawa inahitajiwa kufanya hivyo chini ya sheria za kimataifa.

Korea Kaskazini inafuata mtindo ule ule wake wa ukaidi katika kujibu vikwazo vipya vigumu vya kimataifa vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo kufuatia jaribio lake la nne la nyuklia na kufyetua roketi nyingine ya masafa marefu.

Pyongyang ilifanya uchochezi wake mpya leo asubuhi, ilipofyatua makombora mawili ya masafa ya wastani yenye uwezo wa kusafirisha bomu ya nuklia, kutoka pwani ya mashariki na kufikisha umbali wa kilomita 800 baharini.

Moja ya makombora yake iliyopewa jina la Rodong, yenye uwezo wa kuwasili hadi Japan inaonekana ililipuka kati kati ya safari.

Korea Kaskazini haikutangaza eneo la marufuku ya usafiri wa meli kabla ya kufyetua makombora hayo ingawa inahitajiwa kufanya hivyo chini ya sheria za kimataifa ili kuonya meli ambazo huwenda zikawa zinasafiri katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG