Makombora yaliyotumika Machi 24 kuna uwezekano yalikuwa yameboreshwa ya Hwasong-15 ICBM, na si makubwa ya Hwasong-17 ICBM, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Korea Kusini aliyeongea na Sauti ya Amerika – VOA – siku ya Jumanne.
Televisheni ya taifa ya Korea Kaskazini wiki iliyopita ilitoa video za majaribio zikimuonyesha kiongozi wao Kim Jong Un yeye mwenyewe akielekeza kile kilichodaiwa kuwa majaribio ya hivi karibuni.