Makombora mawili ya Russia yalipiga mji wa Kharkiv nchini Ukraine Jumapili, kulingana na ripoti ya Reuters, nahuku kombora moja likipiga jengo la makazi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumamosi hali inazidi kuwa mbaya Mashariki mwa Ukraine, huku kukiwa na wimbi jipya la mashambulizi ya makombora ya Russia katika mikoa ya Chernihiv, Zaporizhzhia, Dnipro-petrovsk, Kharkiv, Luhansk, Donetsk na Mykolaiv.
Katika hotuba yake ya kila usiku kwa njia ya video, kiongozi huyo wa Ukraine alisema Russia "inazidi kutuma vikosi vyake katika kuvunja ulinzi wetu.
Maafisa wa Ukraine walisema walizima mashambulizi mapya ya Russia kwenye mji wa mashariki wa Bakhmut uliozingirwa siku ya Jumamosi. Zelenskyy aliapa Ijumaa kutoisalimisha Bakhmut. Tutapambana kadri tuwezavyo.”aliongeza.
Katika mazungumzo ya simu Jumamosi, Zelenskyy alijadiliana na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kuhusu hali ya hivi punde nchini Ukraine na wote wawili walikubaliana kuongeza msaada wa kijeshi kutoka Magharibi ili kurudisha nyuma vikosi vya Russia. Pia walijadili uwezo wa muda mrefu wa vikosi vya kijeshi vya Ukraine.