Makao makuu ya chama cha siasa cha United Russia katika mji unaokaliwa kimabavu na Russia wa Polohy, katika mkoa wa Zaporizhzhia, nchini Ukraine yaliharibiwa Ijumaa, gazeti la The Kyiv Independent liliripoti leo Jumamosi.
Meya wa Melitopol Ivan Fedorov alitangaza tukio hilo kwenye mtandao wa Telegram. Federov alisema Warussia waliumizwa sana nje ya jengo hilo. Tukio hilo liliambatana na uchaguzi usio halali katika maeneo yanayokaliwa na Russia nchini Ukraine, alisema.
Russia imedai kutwaa majimbo ya Kherson, Zaporizhzhia, Donetsk na Luhansk ya Ukraine.
Vikosi vya jeshi la Ukraine vinafanya maendeleo ya taratibu dhidi ya safu ya ulinzi ya Russia katika mji wa mashariki wa Robotyne, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi katika maelezo yake ya kila siku ya kijasusi juu ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Forum