Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 17:18

Makanisa 700 yamefungwa nchini Rwanda


Takwimu hizi zimetolewa baada ya wiki mbili tangu zoezi la kufunga makanisa yasiyokidhi mahitaji lilipoanza. Makanisa yaliofungwa ni yale yaliokuwa yakiwabughudhi wananchi kufuatia kero za waumini wakati wa ibada kutokana na vipaza sauti na ngoma suala ambalo wananchi walikuwa wakililalamikia siku zote

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kwamba kuwepo ujenzi holela wa uanzishwaji makanisa hayo ni dalili tosha inayoashiria wananchi waliobweteka na wasio na la kufanya. Alikuwa akizungumza mbele ya viongozi wote wa serikali kwenye kilele cha kikao cha faragha ambacho kilikuwa kwa muda wa siku nne huko jimbo la mashariki.

Rais wa Rwabda, Paul Kagame
Rais wa Rwabda, Paul Kagame

Wacha niwaambie hebu fikiria katika mji kama Kigali ambako watu wanafikia hatua ya kuyafunga makanisa 700 fikiria idadi hiyo. Hivi hayo ni makanisa au visima vya maji? Au ni viwanda vinavyotoa ajira hivi kweli pale Kigali tunavyo viwanda vinavyofikia idadi hiyo? Lakini huu ni ushahidi kwamba tunafanya mambo kiholela na unapoona vitu vikiendeshwa kiholela-holela ujue mfumo mzima umejengwa kiholela”!!

Awali bodi ya taifa ya uongozi ilitoa tamko kuhusu mahitaji kwa wamiliki wa makanisa kuwa na vyeti vya taaluma hiyo suala ambalo wengi walilipinga wakisema kwamba jambo hilo haliwezikani.

Msemaji wa shirikisho la makanisa ya kiroho Mchungaji Innocent Nzeyimana anasema hata wao waliliona tatizo hilo na kuanza kuyashughulikia hayo mahitaji lakini mengine ni magumu na hayawezi kuwekwa kwenye vitendo.

“Tangu tulipochukuliwa uamuzi huu wakuu wa makanisa wamejitahidi kutimiza yale mahitaji lakini kuna mengine ni magumu. Fikiria asilimia 90 ya makanisa hupangisha kwenye maeneo mbalimbali wanaposema hairuhusiwi kufanyia au kuendesha ibada kwenye maghorofa ya kupanga au nyumba za kuishi unategemea watu watasalia wapi wakati zaidi ya asilimia 90 ya makanisa yanapangisha”?

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:02 0:00

Hata hivyo baadhi ya waumini wanasema hata wao waliliona hilo la utitiri wa makanisa haya kuwa kama kero na kwamba uamuzi wa serikali umekuja kwa wakati muafaka.

Mpaka sasa hakuna takwimu zilizokwishatolewa kuhusu idadi kamili ya makanisa yaliyofungwa kote nchini lakini huenda yakafikia mamia kwa maelfu kwa kutumiwa wastani wa hayo yaliofungwa mjini Kigali. Ngazi za dini, zile za mwanzo hata maafisa wa usalama wamekuwa wakifanya mikutano ya hapa na pale kuhakikisha suala hilo linafuatiliwa kwa ukaribu ili kukomesha utitiri huo wa kuzaliwa makanisa ya kipentekosti.

XS
SM
MD
LG