Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amekubali rasmi
uteuzi wa chama cha Demokratik kuwa mgombea urais siku ya Alhamisi kukiwa na wito mkubwa wa kumaliza vita huko Gaza na kupambana na dhuluma kote duniani, akiweka tofauti kubwa na mgombea wa Republikan Donald Trump.
Katika mapambano ya kudumu kati ya demokrasia na udhalimu,
najua ninaposimama na najua Marekani iko wapi,
Harris alisema akimshutumu Trump kwa kuwasujudia madikteta.
Katika usiku wa mwisho, uliosubiriwa sana katika mkutano wa siku nne huko Chicago, Harris, mwenye umri wa miaka 59, aliahidi kufungua njia mpya kusonga mbele huku yeye na Trump, mwenye umri wa miaka 78 wakiingia katika wiki 11 za mwisho za kampeni zilizo na ukaribu mno.
Forum