Rais wa taifa hilo, Alberto Fernandez, alisema katika hotuba kwa taifa, iliyopeperushwa kupitia runinga, kwamba "mtu mmoja alimnyooshea makamu rais bunduki kichwani, na kujaribu kufyatua risasi."
Video ya tukio hilo inaonyesha bunduki ikiwa karibu kugusa uso wa Cristina Fernandez.
Tukio hilo lilitokea wakati makamu wa rais akiwa amezungukwa na wafuasi wake alipokuwa akirejea nyumbani baada ya siku moja mahakamani, ambapo anakabiliwa na tuhuma za rushwa, wakati alipokuwa rais wa Argentina kuanzia 2007 hadi 2015. Amekana mashtaka yote.
Rais Fernandez alisema jaribio la mauaji lilikuwa tukio baya zaidi tangu nchi hiyo kurejea kwa mfumo wa demokrasia mnamo mwaka wa 1983.