Riek Machar katika barua ya kupinga aliyompelekea mpatanishi wa mazungumzo hayo alisema rasimu hiyo ilianzisha taasisi mbadala kuchukua nafasi au kuendeshwa sambamba na zile zilizoanzishwa na makubaliano ya awali ya amani. Aliongeza kuwa mazungumzo ya sasa ya amani yanapaswa kukamilisha na sio kufuta makubaliano ya awali.
Kiongozi huyo wa zamani wa waasi alitia saini mkataba na Rais Salva Kiir mwaka 2018 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano vilivyoua takriban watu 400,000.
Machar na Kiir walikuwa katika pande tofauti katika vita hivyo ambapo Machar aliteuliwa kuwa makamu wa rais baada ya makubaliano ya mwaka 2018. Kundi lake si sehemu ya mazungumzo ya sasa, ambayo ni ya vikundi ambavyo havikujumuishwa katika makubaliano ya mwaka 2018.
Forum