Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:10

Makamu mwenyekiti wa Olimpiki, Kenya, atiwa mbaroni


Makamu rais wa kamati ya Olimpiki nchini kenya amekamatwa kwa shutuma za wizi jana jumatatu, na kutolewa na polisi akiwa amejificha chini ya kitanda.

Amekamatwa kwenye nyumba ambayo ilikuwa imejaa maboksi ya viatu vya kukimbilia vya Nike na vifaa vingine.

Vifaa hivyo vinadaiwa vilikuwa vimeazimiwa kupewa wanariadha waliokuwa wameshiriki michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, ukamataji huo umekuja kutokana na kuchapishwa kwa ripoti za uchunguzi.

Taarifa za uchunguzi ni kwaba zaidi ya dola laki nane zilitengwa kulipia gharama za wanariadha wa Kenya kwenye michezo hiyo.

Vilevile inaelezwa pia kupokelewa vifaa ambavyo vilitolewa na mdhamini kampuni ya Nike lakini viliibiwa na maafisa wa juu wa michezo.

Makamu rais wa kamati hiyo ya kitaifa Ben Ekumbo pia alikuwa mkuu wa shirikisho la Waogoleaji Kenya alikamatwa mjini Nairobi na kikosi cha kurugenzi ya uchunguzi wa kihalifu.

Alikutwa amejificha chini ya kitanda pale polisi walipovamia nyumbani kwake.

XS
SM
MD
LG