Marekani ilitoa ushauri Jumatatu ikizionya kampuni za Marekani kuhusu hatari zinazoongezeka za kufanya biashara na makampuni yanayomilikiwa na serikali na makampuni yanayodhibitiwa na jeshi nchini Sudan.
"Hatari hizi miongoni mwa mambo mengine, ni pamoja na hatua za hivi karibuni zilizofanywa na Baraza Kuu la Sudan na vikosi vya usalama chini ya amri ya jeshi, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya waandamanaji," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema katika taarifa.
Nchi hiyo imekumbwa na maandamano tangu mapinduzi ya kijeshi mwezi Oktoba, na wanasheria wanasema darzeni ya wafungwa wa kisiasa wangali kizuizini.
Wafanyabiashara na watu binafsi wanaoendesha shughuli zao nchini Sudan wanapaswa kuongeza uangalifu unaostahili kuhusiana na masuala ya haki za binadamu na kufahamu hatari zinazoweza kutokea za juu ya heshima yao katika kufanya shughuli za biashara au miamala na makampuni yanayodhibitiwa na jeshi," Price aliongeza.