Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:45

Makamanda wawili wa Al-Shabab watiwa mbaroni


Wanamgambo wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia.
Wanamgambo wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia.
Serikali ya Somalia inasema imewakamata makamanda wawili waandamizi wa kundi la al-Shabab, mmoja wao ni mshukiwa katika bomu ambalo liliuwa zaidi ya watu 20.

Maafisa waliwaonyesha wanaume hao wawili kwa waandishi wa habari jumatatu katika mji wa Qoryoley lakini hawakuyataja majina yao wakielezea kile kwamba ni kusubiriwa uchunguzi zaidi.

Naibu waziri wa usalama Ibrahim Isak Yarrow anaiambia Sauti ya Amerika-VOA, Idhaa ya Kisomali kwamba mtu mmoja anashukiwa kuwa alihusika katika shambulizi la Septemba mwaka 2009 la bomu la kujitoa mhanga kwenye kituo cha walinda amani wa Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.

Shambulizi liliuwa watu 21, watu 17 kati yao ni wanajeshi wa Afrika akiwemo naibu kamanda wa jeshi, Juvenal Niyonguruza kutoka Burundi.

Mtu mwingine aliyekamatwa inasemekana kuwa anatoa mafunzo kwa Amniyat, kitengo cha ngazi ya juu katika kundi la al-Shabab kinachohusika na operesheni za kujitoa mhanga, ujasusi na mauaji.

Vyanzo vinaiambia VOA kwamba operesheni ya kuwakamata watu hao ilifanywa na kitengo maalumu kijulikanacho kama Gaashan au Shield ambacho kilipatiwa mafunzo kwa msaada wa Marekani.
XS
SM
MD
LG