Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:24

Majeshi ya Syria yapiga wakazi wa Aleppo


Eneo la makazi nchini Syria

UNHCR yasema idadi ya wakimbizi imeongezeka

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wameripoti mapigano makali kote nchini humo Jumanne yakiwemo mapigano katika mji mkubwa wa Aleppo. Kundi la kutetea haki za binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza limesema majeshi ya serikali yamepiga vitongoji vya mji wa Aleppo huku wakipambana vikali na waasi mjini humo. Taarifa za kundi hilo ambazo hutegemea mashahidi zinasema majeshi ya rais Bashar al-Assad pia yameshambulia baadhi ya maeneo katika mkoa wa Deraa. Wanaharakati pia wanaripoti mapigano katika mji mkuu wa Damascus na katika mkoa Homs. Wakati huo, huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameleza hofu yake kufuatia mashambulizi makali ya majeshi ya Syria dhidi ya raia. Nalo shirika wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaripoti kuwa idadi ya watu wanaotoroka manyumbani mwao kutoka mji wa Aleppo huko Syria inazidi kuongezeka. UNHCR inasema mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi yanahujumu juhudi za kuwasaidia maelfu ya watu waliotoroka makwao. Shirika hilo linakisia hadi raia laki mbili wametoroka mji wa Aleppo na vitongoji vyake katika siku za karibuni.

XS
SM
MD
LG