Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:28

Majeshi ya Syria yakamata wachochezi wa ghasia


waandamanaji wakipaza sauti kudai kuondolewa kwa rais wa nchi hiyo
waandamanaji wakipaza sauti kudai kuondolewa kwa rais wa nchi hiyo

Wanaharakati wasema wanajeshi walifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwenye miji iliyokuwa chanzo cha ghasia

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema majeshi ya Syria yamewakamata mamia ya watu katika msako wa nyumba hadi nyumba kwenye miji iliyokuwa chanzo cha ghasia jumatatu wakati msako wa jeshi ukienea katika mji mkuu Damascus.

Vifaru vilifanya doria kwenye mitaa katika mwambao wa banias na mji wa kati wa homs ambako mashahidi wanasema majeshi ya usalama yaliuwa watu 14 jumapili.

Milio ya bunduki ilisikika katika kitongoji cha maadamiyeh mjini Damascus.
Makundi ya kutetea haki za binadamu ya Syria yanasema kukamatwa huko kulilenga viongozi wa waandamanaji wanaoipinga serikali na washiriki.

Pia wamesema zaidi ya raia 630 wamekufa katika ghasia hizo tangu zilipozuka machi na wengine takriban ya elfu nane hawajulikani walipo au wamefungwa.

XS
SM
MD
LG