Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:32

Majeshi ya Syria yaharibu makazi na kukamata raia.


Wakimbizi wa Syria wakibeba chakula kwenye kijiji Utueruki karibu na mpaka wa Syria.
Wakimbizi wa Syria wakibeba chakula kwenye kijiji Utueruki karibu na mpaka wa Syria.

Wakimbizi wa Syria wanasema majeshi yamewakamata mamia ya watu katika vijiji karibu na mji wa waasi wa kaskazini wa Jisr al Shughuor huku wakichoma mazao na kuchinja ng’ombe katika eneo hilo.

Takriban wakimbizi 7,000 waliokimbilia nchi jirani ya Uturuki walisema Jumatatu kwamba majeshi ya Syria yalikuwa yakiharibu makazi mashariki mwa nchi na kukamata wanaume wenye umri kati ya 18 na 40. Wengine walieleza juu ya kampeni ya kuchoma na kuharibu mazingira huku watu wenye sare nyeusi wakimwaga mafuta ya taa kwenye mashamba.

Maelfu ya raia wa Syria walibaki katika maeneo ya mpaka wake na Uturuki. Wengi wao wana mifugo na mali nyingine ambazo watalazimika kuacha ikiwa watavuka mpaka.

Waasi wa Syria wanapambana kupata mabadiliko ya kiutawala na wanamtaka rais Bashar al-Assad na serikali yake waondoke madarakani.

XS
SM
MD
LG