Majeshi ya serikali huko Libya yalifanya mashambulizi makali katika mji wa waasi wa Misrata katika siku hiyo hiyo ambayo NATO iliapa kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya kiongozi aliye na misuko suko wa Libya.
Mashahidi wanasema mji huo wa bandari ulishambuliwa vikali jumatano wakati maelfu ya wanajeshi wanaomuunga mkono Gadhafi kusonga mbele kutoka kusini, mashariki na magharibi.
Madaktari na vyanazo vya waasi vimesema mashambulizi ya Misrata yaliuwa watu wapatao 10 na kujeruhi zaidi ya 25.