Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:31

Jeshi la Marekani kuongeza nguvu zake Somalia


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, kulia,akipeperusha bendera ya Somalia katika ikulu Mogadishu. Alhamisi, Feb. 16, 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, kulia,akipeperusha bendera ya Somalia katika ikulu Mogadishu. Alhamisi, Feb. 16, 2017.

Wizara ya Ulinzi imekusudia kuongeza nguvu zake za kijeshi kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab wa Somalia wenye uhusiano na al-Qaida.

Pentagon inanuia kupeleka wanajeshi wa Marekani kupambana kwa karibu zaidi na vikundi vyenye itikadi kali Somalia ambavyo vimekuwa vikipanga mashambulizi dhidi ya Marekani, afisa wa Ngazi ya juu wa Marekani amesema.

Mapendekezo yaliyotumwa White House na wizara hiyo yatakiwezesha kikosi cha operesheni maalumu kuongeza misaada kwa jeshi la kitaifa la Somalia katika juhudi za kupambana na wapiganaji wa al-Shabab katika nchi hiyo iliharibiwa na vita kwenye Pembe ya Afrika, maafisa wamesema.

Wamesema pendekezo hilo litawapa jeshi hilo wepesi wa kuanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya wale wenye itikadi kali inayoonekana kutishia amani.

Juhudi ya kuongeza nguvu za kijeshi Somalia, inakwenda sambamba na ombi pana la Rais Donald Trump, kwa wizara ya ulinzi kuwa na mpango wa kuongeza kasi katika vita dhidi ya kikundi cha Islamic State huko Iraq na Syria, na kuvishinda vikundi vingine vyenye itikadi kali, ikiwemo al-Qaida na washirika wake.

wanamgambo wa al-Shabab
wanamgambo wa al-Shabab

Wasiwasi wa Marekani juu ya al-Shabab umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na vijana wa Kimarekani katika jumuiya za Kisomali kuonekana kusafiri na kujiunga na mafunzo katika kambi za Somalia, ikiongeza wasiwasi kwamba wanaweza kurejea Marekani na kutenda vitendo vya ugaidi.

Somalia ni moja ya nchi zenye Waislamu wengi ambazo zipo katika orodha ya katazo la Trump la wahamiaji alilolitoa mwezi uliopita. Hata hivyo agizo la kiutendaji lilizuiliwa mapema na mahakama za rufaa ya Marekani.

Jenerali Thomas Waldhauser, akitembelea Agadez, NIger. Novemba 1 2016.(Photo par Samantha Reho, U.S. Africa Public Affairs/ Released)
Jenerali Thomas Waldhauser, akitembelea Agadez, NIger. Novemba 1 2016.(Photo par Samantha Reho, U.S. Africa Public Affairs/ Released)

Somalia ni “yenye changamoto ya hali ya juu inayochanganya,” Jenerali Thomas Waldhauser, Mkuu wa Kikosi cha Marekani -Afrika, amesema wakati wa mahojiano na shirika la habari la “The Associated Press.”

Marekani imekuwa “ikijaribu kuiangalia Somalia katika mtizamo mpya, juu ya hatua ambazo inaweza kuchukua siku za usoni,” amesema Jenerali huyo.

Ameongeza kuwa kuwa iko haja ya kulidhoofisha kundi la al-Shabab linaloendelea kufanya mashambulizi kwa muongo mmoja, na kuliwezesha Jeshi la Umoja wa Afrika kulitokomeza kundi hilo.

Lakini Waldhauser alisita kutoa maelezo zaidi juu ya njia mbadala nyingine mpya zilizokuwa zimependekezwa.

XS
SM
MD
LG