Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:28

Majeshi ya Israeli yafanya operesheni kali dhidi ya Wapalestina, raia tisa wauawa


Waombolezaji wakiwa wamebeba miili minane ya Wapalestina wakati wa maziko huko katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin, Jan. 26, 2023.
Waombolezaji wakiwa wamebeba miili minane ya Wapalestina wakati wa maziko huko katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin, Jan. 26, 2023.

Majeshi ya Israeli yamewaua Wapalestina wasiopungua tisa, akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 60 na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa uvamizi kwenye Ukingo wa Magharibi, Alhamisi, maafisa wa afya wa Palestina walisema, wakisisitiza kwamba hiyo ilikua siku mbaya sana katika ukingo huo.

Ghasia zilitokea wakati maafisa wa afya wa Palestina walichoelezea kuwa ni operesheni kubwa wakati wa mchana katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, ngome ya wanamgambo wa Ukingo wa Magharibi ambayo imekuwa ikilengwa kwa takriban mwaka mzima katika uvamizi na ukamataji. Mzozo uliongezeka mwezi huu, huku Wapalestina 29 wakiuawa tangu kuanza kwa mwaka huu.

Haikufahamika mara moja watu wangapi kati ya wale waliouawa Alhamisi walikuwa na uhusiano na makundi yenye silaha.

Mapigano yamekuja wiki kadhaa baada ya serikali mpya ya Israel ya mrengo wa kulia kuingia madarakani, ambayo iliahidi kuchukua msimamo mkali dhidi ya Wapalestina na kuimarisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika ardhi za Wapalestina wenye matumaini ya kuwa na taifa lao.

Mapigano hayo pia yamekuja siku kadhaa kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ambaye anatarajiwa kuwasili katika eneo hilo na kushinikiza hatua zinazoweza kuboresha maisha ya kila siku kwa Wapalestina.

Jeshi la Israel limesema lilikuwa likifanya operesheni zake za nadra nyakati za mchana kwa sababu lilipokea taarifa za kijasusi kwamba kundi la wanamgambo lilikuwa limepanga mashambulizi dhidi ya waisraeli. Mapigano ya bunduki yalizuka, wakati ambapo jeshi lilisema lilikuwa likiwalenga wanamgambo. Mmoja kati ya watu aliyeuawa alitambuliwa na Wapalestina kuwa ni mwanamgambo.

XS
SM
MD
LG