Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:50

Majeshi ya Bgagbo yanashambulia ngome ya Outtara


Wapiganaji wanaomuunga mkono Alassane Outatara.
Wapiganaji wanaomuunga mkono Alassane Outatara.

Watu 462 wameuawa mpaka sasa katika ghasia za baada ya uchaguzi Ivory Coast.

Afisa wa Umoja wa mataifa huko Ivory Coast anasema majeshi yanayomuunga mkono rais aliyepo madarakani Laurent Bgagbo yanafyatua risasi kwa makusudi kwenye maeneo ambayo yanayomuunga mkono mpinzani wake Alassane Outtara.

Afisa wa haki za binadamu Gillaume Ngefa aliumbia mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi kwamba mashambulizi hayo na mengine yameuwa watu wapatao hamsini katika wiki iliyopita ikiwa ni pamoja na watoto watano na kujeruhi darzeni kadhaa.

Ngefa ambaye alikuwa akiongea mjini Abidjan amesema mashambulizi hayo yamesababisha vifo 462 kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Ivory coast.

Serikali ya Bgagbo imekana kutumia silaha kali dhidi ya raia na kulaumu Umoja wa Mataifa kwa kumuunga mkono Bw. Outtara katika mzozo wa Ivory Coast.

XS
SM
MD
LG