Majeshi ya Umoja wa Afrika yamepambana na wanamgambo wa Somalia wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi wa al-qaida huko Mogadishu. Haikujulikana mara moja waliojeruhiwa kwenye mashambulizi ya silaha nzito nzito Jumanne alfajiri. Lakini maafisa wa kijeshi wanasema vikosi vya AU kutoka Burundi vikiungwa mkono na serikali ya mpito ya Somalia vilifanya mashambulizi kwenye ngome za al-shabab nje ya mji wa Mogadishu ili kudhibiti mjihuo wa Somalia. Walisema operesheni hiyo ilikuwa na mafanikio.
Majeshi ya AU yapambana vikali na al-Shabab

Vikosi vya AU vyapambana na Al shaba na kusema vimepata mafanikio.