Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:30

Majenerali wa Marekani na Ukraine wakutana Poland


Jenarali wa jeshi la Marekani, Mark Milley, na mwenzake wa Ukraine, walikutana katika kambi ya kijeshi kusini masharki mwa Poland, Jumanne.

Katika mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana, ikiwa ni ishara ya kukua kwa uratibu wa mataifa hayo mawili kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa miezi 11 wa Russia.

Melley, ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa majeshi ya Marekani, na Jenerali Valerii Zaluzknyi wa Ukraine, walizungumza kwa saa mbili katika mahala ambako hakukutajwa karibu na mpaka wa Ukraine na Poland.

Viongozi hao wawili wa kijeshi hawakuwahi kukutana kabla, lakini wamekuwa wakizungumza toka vikosi vya Russia kuivamia Ukraine, Febuari mwaka jana.

Mkutano huo umefanyika wakati Marekani na washirika wake wa mataifa ya magharibi wakiendelea kutuma mabilioni ya dola ama silaha kwa Ukraine kupambana na Russia.

XS
SM
MD
LG