Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:13

Majaji wa Tunisia waongeza mgomo wao kwa wiki ya pili

Wanasheria na wanaharakati wakikusanyika kwenye ngazi za Ikulu ya Haki wakati wa maandamano huko Tunis, Tunisia, Juni 8, 2022.(AP Photo/Hassene Dridi)
Wanasheria na wanaharakati wakikusanyika kwenye ngazi za Ikulu ya Haki wakati wa maandamano huko Tunis, Tunisia, Juni 8, 2022.(AP Photo/Hassene Dridi)

Majaji wa Tunisia waliongeza mgomo wao kwa wiki ya pili baada ya Rais Kais Saied kukataa kubadili uamuzi wa kuwafuta kazi darzeni ya majaji hao, muungano wa vyama vya majaji ulisema katika taarifa ya pamoja siku ya Jumamosi.

Saied aliwafukuza kazi majaji 57 mwezi huu, akiwashutumu kwa ufisadi na kuwalinda magaidi, madai ambayo Chama cha Majaji wa Tunisia kilisema kuwa mengi yalikuwa na ushawishi wa kisiasa. Mgomo wa kwanza ulianza Juni 4.

Uamuzi wa Saied ulichochea wimbi la ukosoaji wa ndani na nje ya nchi. Mashirika kumi ya haki ya kimataifa yalimshutumu kwa kusababisha pigo kubwa kwa uhuru wa mahakama nchini humo.

XS
SM
MD
LG