Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 23:25

Majaji wa Mahakama ya Juu Marekani wasikiliza hoja kwamba marais wa zamani hawawezi kufunguliwa mashtaka ya jinai


Majaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani inasikiliza hoja kwamba marais wa zamani hawawezi kufunguliwa mashtaka ya jinai
Majaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani inasikiliza hoja kwamba marais wa zamani hawawezi kufunguliwa mashtaka ya jinai

Mahakama ya Juu ya Marekani siku ya Alhamisi ilionekana kushuku madai ya Rais wa zamani Donald Trump kwamba ana kinga kamili ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai kwa vitendo alivyofanya akiwa madarakani

Mahakama ya Juu ya Marekani siku ya Alhamisi ilionekana kushuku madai ya Rais wa zamani Donald Trump kwamba ana kinga kamili ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai kwa vitendo alivyofanya akiwa madarakani lakini majaji kadhaa walionyesha mashaka juu ya maelezo ya mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake katika kesi inayosubiriwa ya serikali kuu.

Trump anakabiliwa na mashtaka ya jinai katika maeneo manne nchini Marekani, lakini kesi iliyojadiliwa siku ya Alhamisi ilikuwa mashtaka yake ya serikali kuu kwa madai kwamba ilikuwa sehemu ya juhudi zake za kutengua ushindi wa Rais Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2020, alifanya udanganyifu dhidi ya serikali ya Marekani. , alijaribu kuzuia shughuli rasmi ya serikali, na kushinikiza maafisa wa umma kinyume cha sheria kumsaidia kuzuia uidhinishaji wa matokeo ya uchaguzi.

Ingawa rais huyo wa zamani angependelea kwa uwazi uamuzi unaokubaliana na madai yake ya kinga katika kila eneo dhidi ya mashtaka ya jinai, uamuzi ambao unachelewesha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kesi yake ya jinai inayoendelea unaweza kumnufaisha yeye pia, kwa kusukuma utatuzi wa kesi hiyo baada ya uchaguzi wa urais nchini Marekani mwezi Novemba. Tutakuletea mengi Zaidi kuhusu kesi hiyo, baadaye katika matangazo haya.

Forum

XS
SM
MD
LG