Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:11

Majaji wa mahakama kuu ya Kenya wakamatwa kwa tuhuma za ufisadi


Waandamanji walalamijia visa vya ufisadi Kenya kwenye picha ya maktaba

Majaji wawili wa mahakama kuu nchini Kenya, Aggrey Muchelule na Said Juma Chitembwe Alhamis jioni wamekamatwa na maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, kwa madai ya kula rushwa kutokana na kesi walizo sikiliza awali jijini Nairobi.

Wawili hao walihojiwa kwa zaidi ya saa mbili na kisha kuachiliwa baadaye, lakini wakili wao, Danstan Omari anaeleza kuwa ni mwendelezo wa hatua za serikali kuminya uhuru wa idara ya mahakama.

Wengine waliofikishwa katika makao hayo kuandikisha taarifa ni pamoja na makarani na madereva wanaofanya kazi kwenye ofisi za majaji zao.

Muchelule ni mojawapo wa majaji waliokosa kuteuliwa kwenye mahakama ya rufaa na rais Uhuru Kenyatta kwa madai ya kuwa na dosari za maadili.

Yeye pia ni miongoni mwa majaji sita kati ya 40 ambao Kenyatta hakupandisha vyeo alipofanya uteuzi huo mwezi Juni mwaka huu. Wengine walioachwa nje ni majaji Professa Joel Ngugi na George Odunga.

Japo vyombo vya habari vya Kenya vinanukuu maafisa wa upelelezi kuwa kuna masuala mazito wanayochunguza dhidi ya majaji hao wawili, wakili wao Danstan Omari anadai kuwa kuna maswala yasioeleweka..

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shutma chungu nzima kwa kuteua majaji 34 na kuwaacha wengine sita bila kuweka wazi sababu za kufanya hivyo, na hii imeonekana kama uminyaji wa uhuru wa idara ya mahakama. Muungano wa mahakimu tayari imeeleza kuwa Kenyatta hana uwezo kisheria wa kuchagua baadhi ya majaji huku akiwaacha wengine.

Baraza la Wanasheria nchini Kenya LSK kupitia rais wake Nelson Havi, limeeleza kuwa hatua ya makachero kuwakamata na kuwaacha bila kuwafungulia mashtaka majaji hao ni kuhujumu na kuminya uhuru wa idara ya mahakama.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG