Hatua hiyo imefanyika siku mbili baada ya vikosi vya Kyiv kuingia katika eneo hilo la kimkakati ambalo Russia ilishikilia baada ya kuanza kwa vita na sasa wamekimbia.
Zaidi ya theluthi tatu ya wakazi 300,000 wamekimbia mji, na kubaki watu 75,000 kuwa chini ya uvamizi wa Russia kabla ya kuondoka vikosi vya Russia wiki iliyopita na vikosi vya Ukraine kuanza kusonga mbele.
Mshauri wa meya wa Kherson, Roman Golovnya, amesema vikosi vya Russia wakati vipo katika eneo hilo vilifanya kila hila kuhakikisha watu waliosalia katika mji wanakabiliwa na hali ngumu.
Vikosi vya Ukraine vina hofu kwamba majengo mengi ya Kherson yanaweza kuwa yameharibiwa sana kama ilivyo katika miji mingine kama vile Mariupol, lakini wameukuta upo madhubuti licha ya kuwa na kiwango kidogo cha usambazwaji wa maji.